- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Wanaume Pia Hupata Saratani Ya Matiti?
Wanaume Pia Hupata Saratani Ya Matiti?
Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.
FAHAMU: Katika kila wagonjwa 100 wa saratani ya matiti maaarufu kama breast cancer, mgonjwa 1 huwa ni mwanaume.
Mara nyingi saratani ya matiti kwa wanaume huwa na matokeo mabaya ukilinganisha na saratani ya matiti kwa wanawake.
Iwapo mwanaume utaona dalili zifuatazo;
Chuchu inatoa maji au damu
Ngozi ya chuchu au eneo linalozunguka chuchu kuwa na rangi nyekundu
Chuchu kuingia ndani
Badiliko lolote kwenye ukubwa wa eneo la kifua/titi
Mishipa ya damu inatokeza kifuani
Peau d’orange, hii ni dalili inayoweza kuashiria saratani ya matiti ambapo ngozi ya matiti inaonekana kama ganda la chungwa (dimples). Hii ni kutokana na kuziba kwa mishipa ya limfu kwenye tishu za matiti na inaweza kuwa dalili ya hatua za juu za saratani ya matiti.
peau d’orange
Unashauriwa uende hospitali bila kupuuzia kwa uchunguzi zaidi.
Kwa elimu zaidi kuhusu saratani ya matiti soma hapa: Zijue Sababu 10 Zinazochangia Kupata Saratani Ya Matiti.
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.