- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Mambo Yanayoweza Kusababisha Uume Kuvunjika (PENILE FRACTURE).
Mambo Yanayoweza Kusababisha Uume Kuvunjika (PENILE FRACTURE).
Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.
Je unafahamu kuwa uume unaweza kuvunjika licha ya kuwa umeundwa na misuli ambayo ni corpus carvenosa na corpus spongiosum?
Tatizo la uume kuvunjika hujulikana kwa kitaalamu kama penile fracture na mara nyingi hutokea uume ukiwa umesimama.
Leo tujifunze baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha uume kuvunjika.
picha ya X-ray kuonesha uume uliovunjika
1) Tendo La Ndoa.
Hii hutokea pale ambapo uume uliosimama unachomoka kutoka ukeni na kugonga maeneo ya karibia na mkundu (anus) au maeneo mengine pembeni ya uke hivyo kupelekea uume kuvunjika, lakini pia baadhi ya mitindo ya kufanya tendo la ndoa humuweka mtu kwenye hatari ya kupata shida hii. Mfano baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba mtindo wa kufanya tendo la ndoa uitwao reverse cow girl sex position unaongeza uwezekano wa uume kuvunjika.
Reverse cow girl sex position
2) Wakati Wa Kupiga Punyeto (energetic masturbation).
Uume unaweza kuvunjika wakati wa kujichua, hii hutokea endapo mpigaji atatumia nguvu nyingi na kupelekea kuukunja uume kwa nguvu hata kuvunjika. Epuka kujichua kwaajili ya afya yako ya uzazi.
Punyeto
Tiba ya uume uliovunjika inahusisha upasuaji.
Upasuaji wa uume uliovunjika
Baadhi ya changamoto zinazotokana na matibabu ya tatizo ilo ni pamoja na:
1) Maumivu wakati wa kudindisha (kusimamisha uume)
2) Kushindwa kusimamisha
3) Uume kupinda
HITIMISHO:
Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: https://isayafebu.com/
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.