Soma Hii Kama Una Upungufu Wa Damu Mwilini.

Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.

Ikiwa una changamoto ya upungufu wa damu mwilini zingatia mambo yafuatayo.

1) Usitumie Kahawa, chai wakati wa kula chakula au kunywa dawa za kuongeza damu kwa sababu kahawa/chai huzuia ufyonzwaji (absorption) wa madini chuma kuingia ndani ya mwili.

kahawa

2) Badala yake tumia vyakula vyenye vitamin C kama vile chungwa, limao , chenza kwa sababu husaidia mwili kufyonza (absorb) madini chuma ya kwa urahisi.

vyakula vyenye vitamin C

Kumbuka:

Unaweza ukawa na ulaji mzuri wa vyakula vyenye madini ya chuma, lakini kwa sababu ya utumiaji wa kahawa/chai madini ya chuma yakashindwa kufyonzwa vyema tumboni, vilevile upungufu wa Vitamin C ukadhoofisha ufyonzwaji wa madini ya chuma mwilini.

HITIMISHO:

Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: HOME | ISAYA FEBU

Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.