- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Ujue Mzunguko Wa Hedhi Wa Wanawake
Ujue Mzunguko Wa Hedhi Wa Wanawake
Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.
Leo tujifunze kuhusu mzunguko wa hedhi kwa mwanamke na mambo yanayoathiri mzunguko wa hedhi kwa mwanamke. Ungana nami katika somo hili.
Kwa kawaida mwanamke mwenye afya ya uzazi ni lazima apate hedhi ya mwezi kila mwezi kwa mpangilio sahihi...
Hapa kuna aina 4 za mizunguko ya hedhi na yote nitaitolea ufafanuzi siku za hedhi ni zipi, siku salama na siku za kubeba ujauzito kwa kila mzunguko...
Mzunguko wa hedhi wa kawaida ni ule wa siku 21 hadi 35 ambapo chini yaan siku 21 au zaidi ya siku 35 hutajwa kama sio mzunguko wa kawaida.
Mambo ya kufahamu kabla ya kuanza somo letu ni kama ifuatavyo:
a) Hedhi hutokea kwa mwanamke yeyote alie sawa kiafya na huashilia tayari amepevuka.
b) Mzunguko wa hedhi umegawanyika katika hatua 3 ambazo ni pamoja na…
1️) Hatua ya kwanza-Kutokwa damu.
Hatua hii huchukua kati ya siku 2 hadi 7
2) Hatua ya pili-Kutengenezwa, kupevuka na kutolewa kwa yai la uzazi.
Hatua hii huchukua kati ya siku 7 hadi 12
3) Hatua ya tatu-Yai kuharibika na kuandaliwa kutolewa ili kupisha yai lingine.
Hatua hii huchukua siku 14 bila kujali urefu wa mzunguko wa mwanamke...
️Hivyo inabidi kujua siku hatari na salama kwanza ili uweze kuratibu na kufahamu mzunguko wako, kisha chukua idadi ya siku za mzunguko wako toa na siku 14.
Siku 14 ni zile za hatua ya tatu ambazo ni sawa kwa kila mwanamke aliye katika mzunguko wa kati ya siku 21 hadi 35…
Kisha siku zitakazobaki zigawe kulingana na idadi ya siku za kutoka damu, yaani kama ifuatavyo:
1) Mzunguko wa siku 21.
Siku ya Kwanza iwe ni tarehe yako ya kuanza hedhi. Ikiwa ni mzunguko wa siku 21
a)1-2 kipindi cha hedhi
b) 3-5 siku salama
c) (6)7,8,9,(10) siku za kushika mimba
d) 11------21 siku salama
2) Mzunguko wa siku 26.
a) 1-3 kipindi cha hedhi
b) 4-8 siku salama
c) (*9)10,11,12(*,13) siku za kushika mimba
d) 14-----26 siku salama
3) Mzunguko wa siku 28.
a) 1-3 kipindi cha hedhi
b) 4-9 siku salama
c) (10*),11,12,13,(14*) siku za kushka ujauzto
d) 15--------28 siku salama
4) Mzunguko wa siku 32.
a) 1-5 kipindi cha hedhi
b) 6-13 siku salama
c) (14*)15,16,17,(18*) siku za kubeba ujauzto
d) 19------32 siku salama
5) Mzunguko wa siku 35.
a) 1-7 kipindi cha hedhi
b) 8-16 siku salama
c) (17*)18,19,20,(21*) siku za kubeba ujauzto
d) 22-----35 siku salama
Kumbuka mzunguko wa hedhi kwa mwanamke unaweza kuathiriwa na mambo mengi kama vile vyakula, msongo wa mawazo, kubadili mazingira, mabadiliko ya homoni, kipindi cha kuugua, matumizi ya baadhi ya dawa mfano postinor2 (p2) na kipindi cha kunyonyesha.
Kwahyo ni vyema kuepuka vitu visivyo vya lazima ili kumudu mzunguko wako vizuri. Ukiwa na swali usisite kuuliza.
Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: HOME | ISAYA FEBU
Ulikuwa nami daktari wako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku jema.