- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Huu Ndio Ugonjwa Unaoshambulia Nywele Za Kwapani (Sehemu Za Siri).
Huu Ndio Ugonjwa Unaoshambulia Nywele Za Kwapani (Sehemu Za Siri).
Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.
Je umeshawahi kukutana na mtu mwenye hali hii hapa chini kwenye picha katika sehemu yake ya kwapa/sehemu za siri?
Trichomycosis
Hali hiyo hapo juu kwenye picha ni ugonjwa hujulikanao kwa kitaalamu kama Trichomycosis (trichobacteriosis).
Trichomycosis ni hali ambayo inahusisha ukuaji wa bakteria kwenye nywele, haswa katika maeneo yenye joto na unyevu kama vile kwapani, kwenye sehemu za siri, au kwenye sehemu zingine za mwili zenye nywele nyingi. Kawaida, hii husababishwa na bakteria aina ya Corynebacterium, na inaweza kuonekana kama mabaka meupe au rangi ya njano kwenye nywele.
Ikiwa ukuaji wa bakteria hutatokea kwenye nywele za kwapani hali hiyo hujulikana kwa kitaalamu kama trichomycosis axillaris lakini pia kama ukuaji wa bakteria hutatokea kwenye nywele za sehemu za siri hali hiyo hujulikana kwa kitaalamu kama trichomycosis pubis.
Dalili Za Ugonjwa Wa Trichomycosis:
Dalili za ugonjwa wa Trichomycosis axillaris ni pamoja na:
Nywele zenye rangi nyeupe, njano au kijani
Kukua kwa utando mwembamba kwenye nywele
Harufu mbaya kwenye eneo husika inayotokana na bakteria
Kuhisi kuwashwa au kuchoma kwenye eneo husika
Matibabu Ya Ugonjwa Wa Trichomycosis:
Matibabu ya ugonjwa huu mara nyingi hujumuisha kuosha eneo lenye tatizo kwa sabuni zenye antibakteria kama vile benzoyl peroxide soap au dawa maalum za kuua bakteria.
Benzoyl peroxide soap
Katika hali zingine, inaweza kuhitajika kutumia dawa ya meno inayozuia bakteria (antibacterial toothpaste) kwenye nywele kwa muda.
dawa ya meno
Ikiwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi, ni muhimu kuonana na daktari ili upate ushauri zaidi na matibabu sahihi.
HITIMISHO:
Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: HOME | ISAYA FEBU
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.