Fahamu Sababu Na Tiba Ya Tatizo La Kukua Kwa Matiti Ya Mwanaume (GYNECOMASTIA).

Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.

Leo tujifunze kuhusu sababu na tiba ya tatizo la kukua kwa matiti ya mwanaume, hali inayojulikana kwa kitaalamu kama Gynecomastia. Ungana nami katika somo hili.

Gynecomastia ni hali ambayo mwanaume anakabiliwa nayo ambapo tishu za matiti hukua na kusababisha kuonekana kwa matiti yenye ukubwa mkubwa au yenye kufanana na ya mwanamke.

Hali hii ya kukua kwa tishu za matiti kwa mwanaume huweza kutokea kipindi cha utotoni,wakati wa balehe pia hata uzeeni.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu za kukua kwa matiti ya mwanaume (gynecomastia), zikiwemo:

1) Kushindwa Kuwiana Kwa Homoni.

Mwanaume pia huzalisha homoni ya estrojeni ambayo husababisha matiti kukua lakini haiwezi fanya kazi sababu ya uwepo wa homoni ya kiume testosteroni, inapotokea estrojeni imekua nyingi kuliko testosteroni hupelekea matiti kukua kwa mwanaume.

2) Kuongezeka Kwa Uzito.

Uzito uliopitiliza hupelekea kuongezeka kwa mafuta mwilini hivyo baadhi ya mafuta huhifadhiwa kwenye matiti hivyo hufanya tishu za matiti kukua, lakini pia uzito kuongeza sana inaweza leta kushindwa kuwiana vizuri hivyo kupelekea gynecomastia.

3) Matumizi Ya Baadhi Ya Madawa.

Baadhi ya dawa zimehusishwa na kupelekea kwa tishu za matiti kukua, dawa hizo ni kama amphetamines, marijuana, opioids pamoja na anabolic steroids ambazo hutumika na wanamichezo wale wanyanyua vyuma vizito kukuza misuli.

Tiba Ya Kukua Kwa Matiti Ya Mwanaume (GYNECOMASTIA).

Tiba ya tatizo la kukua kwa matiti ya mwanaumr ni pamoja na;

1) Kupewa dawa ambazo husaidia kutibu tatizo la homoni kwa kuzirejesha kwenye uwiano sawa.

2) Kufanyiwa upasuaji wa kupunguza ukubwa wa matiti.

3) Kama sababu ilikua ni matumizi ya dawa basi unatakiwa uache matumizi ya dawa hizo ili kuepuka tatizo.

MWISHO: Usomapo makala hii, usisahau kushea kwa wale wote uwapendao ili nao wapate kujifunza.

Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: HOME | ISAYA FEBU

Ni mimi mwenye kujalia afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.