Shahawa Kutoka Ukeni Baada Ya Mshindo.

Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.

Je ukiwa kama ME/KE unajiuliza au kushangazwa na kitendo cha shahawa kutoka ukeni mara baada ya uume kuchomoka wakati wa tendo?

Hali ya kuvuja kwa shahawa kutoka kwenye uke mara baada ya mwanaume kuchomoa uume wake wakati wa tendo la ndoa hujulikana kwa kitaalamu kama effluvium seminis.

Hali hiyo siyo ugonjwa wala siyo sababu ya mwanamke kutokushika mimba (infertility).

Hali hiyo hutokea kulingana na maumbile ya uke.

Kuepuka hali hiyo inashauriwa kuweka mto chini ya makalio kisha miguu iwe ukutani walau kwa dakika tano baada ya mshindo.

Lakini pia ni ishara nzuri kwa mwanaume kuzalisha mbegu za kutosha.

Isipokuwa mwanaume ambae hushiriki tendo la ndoa mara kwa mara, mbegu za kiume zitakosa muda wa kukomaa (No Time for Maturation).

HITIMISHO:

Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: HOME | ISAYA FEBU

Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.