Sababu Za Uke Kuwa Mkavu Wakati Wa Tendo La Ndoa.

Uke kuwa mkavu wakati wa tendo la ndoa ni hali ambapo uke hauzalishi ute wa kutosha ukeni, hali ambayo inaweza kusababisha maumivu, na michubuko wakati wa kujamiiana.

Tatizo la ukavu ukeni hujulikana kwa kitaalamu kama vaginal dryness.

Ukavu Ukeni Husababishwa Na Nini?

Uke kuwa mkavu wakati wa tendo la ndoa kunaweza kutokea kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu kuu zinazoweza kusababisha ukavu ukeni ni pamoja na:

1) Ukosefu Wa Msisimko Wa Kutosha Kabla Ya Tendo La Ndoa.

Ikiwa mwanamke hajapata msisimko wa kutosha au maandalizi kabla ya tendo la ndoa (foreplay), ute wa asili kutoka ukeni hauwezi kutengenezwa ipasavyo. Hii inaweza kusababishwa na uchovu, msongo wa mawazo kwa mwanamke.

2) Msongo Wa Mawazo.

Msongo wa mawazo unaathiri homoni za mwili na unaweza kupunguza hamu ya tendo la ndoa.
Msongo unaweza kusababisha mwili kutokuwa na uwezo wa kuzalisha ute wa asili ukeni, hivyo kusababisha ukavu ukeni wakati wa tendo la ndoa.

3) Matumizi Ya Dawa.

Baadhi ya dawa, hasa antidepressants (dawa za kupunguza msongo wa mawazo), antihistamines (dawa za aleji), na dawa za saratani (chemotherapy), zinaweza kupunguza ute ukeni na kusababisha ukavu ukeni wakati wa tendo la ndoa.

4) Mabadiliko Ya Homoni.

Mabadiliko ya homoni yanayochangia ukavu ukeni wakati wa tendo la ndoa hutokea katika vipindi vifuatavyo:

A) Ukomo Wa Hedhi.

Wanawake wanaoingia katika kipindi cha ukomo wa hedhi (menopause) wanakutana na mabadiliko katika mfumo wao wa homoni, hususan kupungua kwa homoni ya estrojeni, ambayo inaweza kusababisha ukavu ukeni.

Ukavu huu hutokea kwa kawaida miaka mingi baada ya hedhi kuacha kabisa, lakini pia unaweza kutokea wakati wa perimenopause, kipindi cha kabla ya ukomo wa hedhi.

Kadri umri unavyoongezeka, viwango vya homoni ya estrojeni hupungua, jambo linaloweza kusababisha ukavu ukeni, hasa kwa wanawake walio kwenye umri wa ukomo wa hedhi (miaka 45-55).

 B) Kunyonyesha.

Wanawake walioko kwenye kipindi cha kunyonyesha wanaweza kushuhudia kupungua kwa unyevunyevu wa uke kutokana na kupungua kwa homoni ya estrojeni.


C) Matumizi Ya Vidonge Vya Uzazi Wa Mpango.

Baadhi ya aina za vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kupunguza homoni ya estrogeni, na hivyo kusababisha ukavu ukeni.

5) Matatizo Ya Kiafya.

Magonjwa kama vile kisukari, ugonjwa wa Sjögren’s syndrome, na matatizo mengine ya afya yanaweza  kusababisha mwili kutokuwa na uwezo wa kuzalisha ute wa asili ukeni, hivyo kusababisha ukavu ukeni wakati wa tendo la ndoa.

6) Kutumia Bidhaa Za Kusafisha Uke (Douching).

Kuosha uke kwa kemikali au sabuni maalum (Douching) kunaweza kuharibu usawa wa bakteria na pH ya uke, na hivyo kusababisha ukavu ukeni pamoja na hatari ya maambukizi ya uke.

Jinsi Ya Kuondoa Ukavu Ukeni:

Ili kuondoa tatizo la ukavu ukeni, mwanamke unashauriwa kufanya mambo yafuatayo:

1) Matumizi Ya Vilainishi.

Matumizi ya vilainishi (lubricants) vya maji au vya asili kama vile mafuta ya nazi vinaweza kusaidia kupunguza ukavu wa uke wakati wa tendo la ndoa.

Weka kiasi kidogo cha lubricant ukeni kabla ya tendo la ndoa ili kuongeza unyevunyevu na kupunguza maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa. Epuka kutumia mate kama kilainishi wakati wa tendo la ndoa kwani kunaongeza hatari ya kupata maambukizi ukeni.

2) Kufanya Foreplay (Maandalizi Ya Mapenzi) Kwa Muda Mrefu.

Foreplay ni muhimu ili kuongeza msisimko kabla ya tendo la ndoa. Muda mrefu wa foreplay husaidia mwili kuzalisha unyevunyevu wa asili kwa wingi, hivyo kupunguza ukavu ukeni.

Muda wa kupeana mapenzi ya kimahaba kama vile kubusu, kutomasana, na kuzungumza unaweza kusaidia kuamsha mwili na kuongeza unyevunyevu.

3) Kunywa Maji Ya Kutosha.

Kukosa maji ya kutosha mwilini kunaweza kupunguza unyevunyevu ukeni. Kunywa maji mengi kila siku ili kusaidia mwili kuzalisha unyevunyevu wa kutosha, ikiwa ni pamoja na ute wa uke.

4) Tiba Ya Homoni (Hormone Therapy).

Ikiwa ukavu wa uke unahusiana na kupungua kwa homoni ya estrojeni (hasa kwa wanawake waliokoma hedhi), daktari anaweza kupendekeza tiba ya homoni, kama vile krimu za estrojeni (estradiol vaginal cream) au vidonge vya estrojeni.

Tiba hii inaweza kusaidia kuongeza unyevunyevu ukeni na kuboresha hali ya uke.

5) Epuka Kutumia Bidhaa Zenye Kemikali Kali Ukeni.

Epuka kutumia sabuni zenye manukato, douching, au bidhaa nyingine zenye kemikali kali ambazo zinaweza kuvuruga pH ya uke na kupunguza unyevunyevu wa asili ukeni.

6) Epuka Msongo Wa Mawazo.

Msongo wa mawazo unaweza kupunguza hamu ya tendo la ndoa na kusababisha uke kuwa mkavu. Fanya mazoezi, yoga, meditation, au kutembea mara kwa mara ili kupunguza msongo wa mawazo.

Dawa Ya Asili Ya Kuondoa Ukavu Ukeni:

By the way, hivi unajua kwamba dawa ya asili iitwayo PANACEA iliyotengenezwa kutokana na mimea  na matunda dozi nzima ya wiki 2 yenye thamani ya TZS 85,000/= itakusaidia kutatua changamoto yako ya uke kuwa mkavu?

NDIYO ni kweli, kupata dawa hiyo wasiliana nasi kwa kubonyeza kitufe (button) kifuatacho hapa chini, tunapatikana Makulu-Dodoma mjini.

HITIMISHO:

Ikiwa tatizo hili la uke kuwa mkavu linaendelea au linakuleta usumbufu wakati wa tendo la ndoa, ni vyema kushauriana na mtaalamu wa afya ya uzazi ili kupata uchunguzi na matibabu yanayofaa.