- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Sababu Za Mwanaume Kuwahi Kumwaga.
Sababu Za Mwanaume Kuwahi Kumwaga.
Kuwahi Kumwaga:
Kuwahi kumwaga (kuwahi kufika kileleni) kwa mwanaume ni hali ambayo hutokea pale mwanaume anapopata mshindo (anapofika kileleni) mapema zaidi kuliko yeye au mwenza wake wanavyotarajia, mara nyingi ndani ya dakika chache baada ya kuanza tendo la ndoa.
Tatizo hili hujulikana kwa kitaalamu kama premature ejaculation.
Hili ni tatizo linalowakumba wanaume wengi kwa nyakati tofauti za maisha yao jambo ambalo hupelekea kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada ya hali hii kutokea.

Sababu Za Kuwahi Kumwaga:
Tatizo hili husababishwa na mambo mbalimbali ya kisaikolojia, kibailojia, na mtindo wa maisha.
A) Sababu Za Kisaikolojia:
Sababu za kisaikolojia zinazochangia tatizo hili ni pamoja na:
1) Hofu Ya Kushindwa (Performance Anxiety).
Mwanaume anapokuwa na hofu ya kutomridhisha mwenzi wake, anaweza kujikuta akifikia mshindo haraka zaidi.

2) Wasiwasi Wakati Wa Tendo La Ndoa.
Wasiwasi kuhusu utendaji wa tendo la ndoa unaweza kumfanya mwanaume amalize haraka bila kutarajia.

Mwanaume akiwa na historia ya kupata hali hii kabla, huwa anapoteza kujiamini na kuwa na wasiwasi kwamba hali hiyo itatokea tena na matokeo yake husababisha kumaliza mapema (kuwahi kufika kileleni).
3) Msukumo Wa Kisaikolojia (Psychological Conditioning).
Ikiwa mwanaume amekuwa na tabia ya kufanya mapenzi kwa haraka (kwa mfano, katika mazingira yasiyo salama au ya haraka), mwili wake unaweza kuzoea kufika kileleni mapema.

4) Msisimko Mkubwa Kupita Kiasi.
Ikiwa mwanaume ana msisimko mkubwa sana, hasa kwa mpenzi mpya au baada ya muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa, anaweza kuwahi kufika kileleni.
5) Tabia Ya Kujichua Mara Kwa Mara (Masturbation).
Mara nyingi mwanaume anayejichua (kupiga punyeto) huwa anafanya haraka kwa kujificha ili asikutwe na mtu hivyo mwili wake unaweza kuzoea kufika kileleni haraka hata wakati wa tendo la ndoa.

B) Sababu Za Kibailojia:
Sababu za kibailojia zinazochangia tatizo hili ni pamoja na:
1) Mabadiliko Ya Homoni.
Kiwango cha chini cha serotonin (homoni inayodhibiti mshindo) kinaweza kufanya mwanaume amwage haraka zaidi.

2) Magonjwa Au Matatizo Ya Kiafya.
Magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la juu la damu, matatizo ya tezi dume, au matatizo ya mfumo wa neva yanaweza kuchangia hali hii.
Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu: Mfumo wa neva unadhibiti hisia na msisimko; ikiwa kuna hitilafu yoyote, inaweza kusababisha kumaliza mapema (kuwahi kufika kileleni).
C) Sababu Zinazotokana Na Mtindo Wa Maisha:
Sababu zinazotokana na mtindo wa maisha ni pamoja na:
1) Kutofanya Mazoezi.
Misuli dhaifu ya nyonga (pelvic floor muscles) inaweza kusababisha mwanaume kushindwa kuchelewesha mshindo.
2) Unywaji Wa Pombe Kupita Kiasi Na Uvutaji Wa Sigara.
Hivi vyote huathiri mzunguko wa damu na neva zinazodhibiti mshindo. Lakini pia matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo cocaine, amphetamine huchangia tatizo hili.

3) Uchovu na Kutopumzika vya Kutosha.
Mwili mchovu hauna uwezo wa kudhibiti msisimko ipasavyo, hivyo kusababisha kumwaga haraka.
Njia Za Kudhibiti Kuwahi Kumwaga:
Ikiwa mwanaume unasumbuliwa na changamoto ya kuwahi kumwaga wakati wa tendo la ndoa unashauriwa kufanya mambo yafuatayo:
1) Mazoezi Ya Kudhibiti Misuli Ya Nyonga (Pelvic Floor Exercises/Kegel Exercises).
Mazoezi haya husaidia kuimarisha misuli inayodhibiti utoaji wa shahawa na kusaidia kuchelewesha kufika kileleni.

2) Tekniki Ya “Stop And Start”.
Wakati mwanaume anakaribia kufika kileleni, anaweza kusimama kwa sekunde chache, kupunguza kasi, na kisha kuendelea. Hii husaidia kuongeza udhibiti wa mwili.
3) Tekniki Ya “Squeeze”.
Kabla ya kufika kileleni, mwanaume anaweza kubana uume wake kwa mkono ili kupunguza Msisimko Na Kuchelewesha Kumaliza.
4) Kupunguza Msongo Wa Mawazo.
Mazoezi ya kupumzika kama vile yoga, meditation, au hata kupunguza hofu ya kutomridhisha mpenzi yanaweza kusaidia.
5) Kubadilisha Mkao Wa Tendo La Ndoa.
Baadhi ya mikao husaidia kudhibiti kasi ya kufika kileleni. Mkao wa mwanamke kuwa juu mara nyingi husaidia mwanaume kudhibiti harakati zake.

6) Matumizi Ya Kondomu.
Kondomu husaidia kupunguza hisia za moja kwa moja kwenye uume, hivyo kuchelewesha kufika kileleni.
7) Tiba Ya Dawa Au Ushauri Wa Daktari.
Ikiwa tatizo ni sugu, daktari anaweza kupendekeza dawa maalum kama dapoxetine, au tiba ya kisaikolojia kama CBT (Cognitive Behavioral Therapy).
Tiba Ya Asili Ya Kuchelewa Kufika Kileleni.
By the way, hivi unajua kwamba dawa ya asili iliyotengenezwa kutokana na mimea na matunda iitwayo PANACEA, dozi nzima ya wiki 2 yenye thamani ya TZS 85,000/= itakusaidia kutatua changamoto yako ya kuwahi kufika kileleni?

NDIYO ni kweli, kupata dawa hiyo wasiliana nasi kwa bonyeza kitufe (button) kifuatacho hapa chini, tunapatikana majengo sokoni, Dodoma mjini.
HITIMISHO:
Kuwahi kumwaga wakati wa tendo la ndoa ni tatizo linaloweza kurekebishwa kwa kufanya mazoezi, kubadili mtindo wa maisha, na kuzingatia afya ya akili na mwili. Ikiwa hali hii inaathiri mahusiano au kuleta msongo wa mawazo, ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu.