Mwanaume Mwenye Korodani Moja Anaweza Kuzalisha?

Ndiyo, mwanaume mwenye korodani moja bado anaweza kuzalisha. Korodani ina jukumu la kuzalisha mbegu za kiume (sperms) na homoni ya testosterone, ambayo ni muhimu kwa uzazi.

Kwa kawaida, mwanaume huwa na korodani mbili, lakini kuwa na moja pekee—iwe ni kwa sababu ya kuondolewa kwa njia ya upasuaji (orchidectomy), jeraha, au kuzaliwa hivyo (cryptorchidism)—hakuathiri uwezo wa kuzalisha mradi korodani iliyobaki inafanya kazi vizuri.

Korodani moja yenye afya inaweza kutengeneza kiwango cha kutosha cha mbegu za kiume na testosterone kumwezesha mwanaume kupata mtoto.

Soma pia hizi makala: