- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Haya Ndio Matatizo 7 Yanayoambatana Na Unene Uliopitiliza.
Haya Ndio Matatizo 7 Yanayoambatana Na Unene Uliopitiliza.
Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.
Je unajua ukiwa mnene kupitiliza unakuwa kwenye hatari ya kupata matatizo ya kiafya? Jibu ni NDIYO.
unene uliopitiliza
Leo tujifunze kuhusu baadhi ya matatizo yanayoambatana na unene uliopitiliza. Ungana nami katika somo hili.
Hali ya kuwa na unene uliopitiliza inayojulikana kwa kitaalamu kama "obesity," ni tatizo linalokua duniani kote na linaweza kuwa na athari kubwa za kiafya.
Kutokana na baadhi ya watu kuwa na mitindo mibovu ya maisha ( (poor lifestyles) kumekua na ongezeko la watu wenye unene uliopitiliza hivyo Kuwaweka kwenye hatari ya kupata matatizo mbali mbali ya kiafya ambayo ni pamoja na:
1) Kisukari.
Takwimu zinaonesha kwamba katika kila watu 10 wenye kisukari aina ya pili (Type 2 diabetes), watu 9 kimetokana na unene uliopitiliza. Hii inasababishwa na kuwepo kwa mafuta mengi mwilini pia kushindwa kuwiana kwa uzito wa mwili (kuwa na BMI kubwa).
Kisukari ni ugonjwa hatari ambao husababisha vifo vya watu wengi duniani hasa katika nchi zinazoendelea.
diabetic foot ulcer (DFU)
2) Magonjwa ya moyo.
Unene uliopitiliza husababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu ili kufikisha damu sehemu mbali mbali za mwili pia, hivyo wepo wa mafuta kwenye mishipa ya damu husababisha moyo kushindwa kusukuma damu vizuri hivyo kupelekea kupata matatizo ya moyo kama vile moyo kufeli (heart failure), shambulio la moyo (heart attack) n.k
3) Matatizo ya uzazi.
Tafiti zinaonesha kwamba baadhi ya matatizo ya uzazi kama vile upungufu wa mbegu za kiume (low sperm count), mbegu za kiume zenye shida (abnormal sperm morphology), kushindwa kusimamisha (erectile dysfunction) hutokana na unene ulipotiliza.
4) Matatizo ya ini na figo.
Uwepo wa mafuta mengi mwilini husababisha baadhi ya mafuta kuhifadhiwa kwenye ini hivyo kusababisha tatizo la ini (non alcoholic fatty liver disease).
5) Kiharusi.
Watu wenye unene kupitiliza wako kwenye hatari kubwa ya kupata kiharusi (stroke), hasa kama wana viwango vya juu vya cholesterol na shinikizo la juu la damu.
6) Matatizo ya Pumzi.
Unene kupitiliza unaweza kusababisha shida za kupumua kama vile sleep apnea ambapo mtu anakosa kupumua kwa muda mfupi wakati wa usingizi.
7) Shida za Kibofu cha Mkojo,
Unene kupitiliza unaweza kusababisha shida za kibofu cha mkojo, kama vile kushindwa kudhibiti mkojo (urinary incontinence).
HITIMISHO:
Hayo hapo juu ni matatizo machache miongoni mwa matatizo mengi yanayotokana na unene uliopitiliza. Lakini pia tatizo la unene kupitiliza linaweza kuepukika kwa kuanza na kubadili kwanza mtindo wa maisha ukianza na ulaji wa lishe bora, pili kufanya mazoezi husaidia kuepuka tatizo ilo.
Usomapo makala hii usisahau pia kushea kwa wale wote uwapendao ili nao wapate kujifunza.
Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: HOME | ISAYA FEBU
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.