Haya Ndio Mambo 4 Yanayohatarisha Afya Ya Ini Lako.

Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.

Leo tujifunze kuhusu ini na mambo yanayohatarisha afya ya ini lako. Ungana nami katika somo hili.

Ini ni kiungo muhimu sana ndani ya miili yetu, hufanya kazi zaidi ya 500, moja ya kazi ni kuchuja na kuondoa sumu kutoka kwenye damu.

Ini ni kiungo cha pili mwilini kwa ukubwa baada ya ngozi ikiwa na wastani wa uzito wa 1.2kg-1.5kg.

Kutokana na sababu mbalimbali hatarishi, ini hupata shida na kuvimba na kushindwa kufanya kazi vizuri. hii hali huitwa HOMA YA INI Au HEPATITIS.

Yafuatayo ni mambo yanayohatarisha afya ya ini lako, yakiwemo:

1) Matumizi Holela Ya Dawa Bila Ushauri Wa Daktari.

Utumiaji holela wa baadhi ya vidonge vikiwemo vya kuondoa maumivu (pain killers) kama aspirin na acetaminophen huongeza hatari kwa mtumiaji kupata matatizo ya ini, pia matumizi ya dawa za kuzuia uvimbe zisizo kua na steroid kama vile ibuprofen.

2) Kuingiza Kemikali Zenye Sumu Ndani Ya Mwili Mara Kwa Mara.

Ini hufanya kazi ya kuchuja sumu mwilini (detoxification), hivyo sumu inapozidi mwilini hupelekea ini kupata shida, kemikali hizo ni kama vile vinyl chloride inayopatikana kwenye plastic na carbon tetrachloride.

3) Matumzi Ya Pombe Kupita Kiasi.

Ini hutumika katika kuchakata pombe ili iweze kutolewa nje ya mwili hivyo matumizi ya pombe yaliokithiri hupelekea seli za ini (hepatocytes) kuharibika, tafiti zinaonesha kwamba katika kila vifo vitano vinavyosababishwa na magonjwa ya ini vinne vinatokana na matumizi ya pombe yaliyokithiri.

4) Muingiliano Wa Vimiminika Vya Mwili Kutoka Kwa Mtu Mwenye Maambukizi Ya Ini.

Baadhi ya magonjwa ya ini husababishwa na virusi wanaopatikana kwenye vimiminika vya mwili kama vile damu na mate, mgusano wa vimiminika hivyo mfano kupitia denda (deep kissing) huongeza hatari ya kupata maambukizi kwenye ini kama vile homa ya ini A&B (Hepatitis A&B).

HITIMISHO:

Ni muhimu kuzingatia afya ya ini kwa kuepuka hayo mambo hatarishi hapo juu na kudumisha mtindo wa maisha wenye afya, pamoja na kufanya uchunguzi wa mara kwa mara (health checkup) ili kuhakikisha afya bora ya ini lako.

Usomapo makala hii usisahau pia kushea kwa wale wote uwapendao ili nao wapate kujifunza.

Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: HOME | ISAYA FEBU

Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.