- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Madhara Ya Bawasiri Kwa Mwanamke.
Madhara Ya Bawasiri Kwa Mwanamke.
Bawasiri ni ugonjwa unaotokea pale ambapo mishipa ya damu kwenye eneo la haja kubwa huvimba na kusababisha maumivu, muwasho, au kutokwa na damu hasa wakati wa kujisaidia haja kubwa. Bawasiri hujulikana kwa kitaalamu kama Hemorrhoids.
Bawasiri inaweza kutokea ndani ya rektamu (bawasiri ya ndani) au nje karibu na mkundu (bawasiri ya nje).

Leo katika mada yetu ya ukurasa huu tutazungumzia baadhi ya madhara ya bawasiri kwa mwanamke. Ungana nami katika kuchambua madhara haya.
1) Kuathiri Shughuli Za Kila Siku Za Mwanamke.
Wanawake wanaougua bawasiri wanaweza kupata maumivu makali na usumbufu wakati wa kujisaidia choo, hali ambayo inaweza kupunguza uwezo wa kufanya shughuli zao za kila siku, kama vile kukaa, kusimama, na kutembea bila raha
2) Upungufu Wa Damu (Nadra Kutokea).
Bawasiri inaweza kusababisha damu kutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa, jambo ambalo linaloweza kuleta upungufu wa damu (anemia) iwapo itaendelea kwa muda mrefu.
3) Athari Za Kisaikolojia.
Mwanamke anaweza kujiskia aibu, au kujisikia vibaya kutokana na hali hii, hasa ikiwa inasababisha harufu mbaya au uchafuzi wa nguo ya ndani (chupi). Hali hii inaweza pia kupunguza kujiamini, kuathiri uhusiano wa kimapenzi na kuleta msongo wa mawazo kwa mwanamke.
HITIMISHO:
Ikiwa una dalili za bawasiri, ni vyema kumuona daktari kwa ushauri zaidi na matibabu sahihi.
Kujifunza zaidi kuhusu bawasiri kwa wanawake bonyeza hapa: Lijue Tatizo La Bawasiri Kwa Wanawake.