Yajue Maambukizi Ya HPV, Saratani Ya Mlango Wa Kizazi Na Kinga Yake.

Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.

Leo tujifunze kuhusu maambukizi ya HPV, saratani ya mlango wa kizazi na Kinga yake.

HPV ni nini ?

HPV ni kifupisho cha "Human Papilloma Virus, hii ni familia ya virusi inayosababisha maambukizi kwenye ngozi, sehemu za uke, uume, mdomo, na koo.

Baadhi ya aina za HPV zinaweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi, koo, au viungo vya uzazi.

Human papilloma virus

Kama ilivyo virusi vingine, HPV husababisha maambukizi kwa kuingia ndani ya seli.

Mara baada ya kuingia ndani ya seli, HPV huteka na kuchukua udhibiti wa shughuli za ndani ya seli na kutumia seli zetu kuzaliana.

Maambukizi ya HPV ni mchakato wa polepole.

Maambukizi ya HPV yanaweza kusababisha mabadiliko kwenye seli ambayo yanaweza kusababisha saratani baada ya muda, ikiwa ni pamoja na saratani ya mlango wa kizazi.

Ukubwa wa maambukizi ya HPV:

Maambukizi ya HPV ni maambukizi yanayoathiri watu wengi sana na yanaenezwa kwa njia ya kujamiiana.

Kwa njia zipi HPV huenezwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine?

  • Kuna takriban aina 40 za HPV ambazo kwa kawaida huambukiza viungo vya uzazi.

  • Aina hizi za HPV husambazwa kwa kugusana ngozi kwa ngozi wakati wa kufanya mapenzi.

  • Maambukizi ya HPV mara nyingi hayana dalili wala ishara.

  • Watu wenye maambukizi ya HPV kawaida hawajui kuwa wanayo.

✍️Hii ni sababu moja ambayo HPV huenea kwa urahisi.

Vipi unaweza kujilinda dhidi ya maambukizi ya HPV?

  • Unaweza kujilinda dhidi ya maambukizi ya HPV kwa kupata chanjo ya HPV.

  • Chanjo hiI ni salama na ina ufanisi na inalinda dhidi ya aina za HPV ambazo ni chanzo cha saratani ya mlango wa kizazi na saratani nyingine kama ya koo, sehemu ya haja kubwa na saratani ya uke.

Linapokuja suala la HPV, lini maambukizi yanaweza kusababisha saratani?

  • Maambukizi ya HPV yanaweza kudumu kwa muda mrefu.

  • Maambukizi ya muda mrefu na aina ya HPV yanaweza kugeuka kuwa saratani.
    Kawaida huchukua miaka kwa hili kutokea.

Aina zipi za maambukizi ya HPV husababisha saratani?

Saratani

Maambukizi ya HPV mdomoni

  • Kesi nyingi za saratani zinazohusiana na HPV husababishwa na aina mbili tu zenye hatari kubwa za HPV: aina ya 16 na aina ya 18.

Inachukua muda gani kwa saratani ya mlango wa kizazi kuendelea?

  • Inaweza kuchukua miaka 3 hadi 7 kwa mabadiliko fulani kwenye seli za mlango wa kizazi kuwa saratani.

  • Lengo la uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi ni kugundua mabadiliko haya wakati yanaweza kutibiwa kwa urahisi bado.

Je, chanjo ya HPV ni salama na ina ufanisi?

Chanjo ya HPV

Ndio, chanjo ya HPV ni njia salama na yenye ufanisi ya kulinda dhidi ya magonjwa yanayohusiana na HPV.

  1. Chanjo ya HPV ina ufanisi sana wakati inapewa kabla ya binti haajaanza kufanya ngono.

  2. Mamilioni ya wanawake ulimwenguni ikiwemo wamepata chanjo ya HPV bila athari mbaya.

Unatakiwa kupata chanjo ya HPV lini?

  • Chanjo inafanya kazi vizuri zaidi wakati inapofanywa kabla ya mtu kuanza kujamiiana na kuwa wazi kwa HPV.

  • Umri bora kwa chanjo ya HPV kwa wasichana kuanzia miaka 9 na hadi miaka 14.

Ni maudhi ya gani huweza kutokea ukipata chanjo ya HPV?

Athari ya kawaida ya chanjo ya HPV inayoweza kutokea ni maumivu na kuvimba mahali ambapo sindano imetolewa.

Kwa Tanzania hatujapata ripoti za athari mbaya za chanjo hii.

HITIMISHO:

Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: https://isayafebu.com/

Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.