Kutokwa Na Shahawa Kwenye Uume Wakati Wa Haja Ndogo/Baada Ya Haja Kubwa.

Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.

Je unatokwa na shahawa kwenye uume wako wakati wa haja ndogo/baada ya haja kubwa?

shahawa

Hali ya kutokwa na shahawa kwenye uume wako wakati wa haja ndogo (baada ya tendo la ngono) au muda mwingine baada ya haja kubwa hujulikana kwa kitaalamu kama semen leakage. Hali hii inaweza kusababishwa na sababu kadhaa zikiwemo:

1) Saratani Ya Tezi Dume.

Hii ni aina ya saratani inayotokea katika tezi ya kibofu cha mkojo (tezi dume), tezi dume inapatikana chini ya kibofu cha mkojo na inazalisha sehemu ya majimaji yanayounda shahawa.

Saratani ya tezi dume inaweza kusababisha kutokwa na shahawa wakati wa haja ndogo/kubwa.

2) Prostatitis.

Hii ni hali inayohusisha kuvimba kwa tezi dume. Tezi dume inazalisha sehemu ya majimaji yanayounda shahawa. Hivyo, hali ya kuvimba kwa tezi dume inaweza kuchangia kutokwa na shahawa wakati wa haja ndogo/kubwa.

3) Retrograde Ejaculation.

Hii ni hali ambapo shahawa badala ya kutoka nje ya uume wakati wa kufika kileleni, inarudi nyuma kuingia kwenye kibofu cha mkojo. Hii inaweza kusababisha kuonekana kwa kiwango kidogo cha shahawa au kutokuwepo kwa shahawa kabisa wakati wa kujamiana, na badala yake kuiona kwenye mkojo baada ya tendo la ngono.

4) Matumizi Ya Dawa.

Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile dawa za mfadhaiko (antidepressants) mfano SSRTIs (selective serotonin reuptake inhibitors), dawa za vidhibiti hisia (mood stabilizers), na baadhi ya matibabu ya homoni pia yanaweza kusababisha kutokwa na shahawa wakati wa haja ndogo/kubwa ikiwa ni matarajio ya matumizi yake (side effects).

HITIMISHO:

Ikiwa una wasiwasi kuwa majimaji yanayotoka kwenye uume si shahawa lakini utokaji wake unahusiana na jeraha au maambukizi, kama vile STI, unapaswa kuonana daktari mara moja kwa ajili ya vipimo na kupata matibabu.

Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: HOME | ISAYA FEBU

Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. isaya Febu, nikutakie siku nj