Kwanini Mtu Mwenye Kisukari Kidonda Chake Hakiponi Haraka?

Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.

Hivi umeshawahi kujiuliza kwanini mtu mwenye kisukari kidonda chake hakiponi haraka?

diabetic foot ulcer (DFU)

JIBU: Kuna sababu kuu mbili za kisukari kuchelewesha kupona kwa vidonda:

KWANZA: Viwango vya juu vya sukari kwenye damu.

Viwango vya sukari kwenye damu vikiwa juu, vinaweza kuharibu mishipa ya damu na neva mwilini. Hii inaweza kusababisha mzunguko wa damu kuwa mbovu kwenye viungo, hasa kwenye miguu na vidole.

Mzunguko mbovu wa damu unamaanisha kuwa majeraha hayatapata oksijeni na virutubisho vinavyohitajika kupona vizuri.

Vilevile, viwango vya juu vya sukari kwenye damu vinaweza pia kudhoofisha mfumo wa kinga, na hivyo kufanya iwe vigumu kwa mwili kupambana na maambukizi.

PILI: Mfumo dhaifu wa kinga ya mwili.

Kisukari kinaweza kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili, na hivyo kufanya iwe vigumu zaidi kupambana na bakteria ambao husababisha maambukizi kwenye majeraha.

Udhaifu wa kinga unatokana na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na viwango vya juu vya sukari kwenye damu huweza kuathiri utendaji wa seli nyeupe za damu.

HIVYO: Ukiwa na kisukari, ni muhimu kuwa mwangalifu zaidi kuhusu kuangalia miguu yako. Chunguza kama una michubuko, au vidonda. Hata jeraha ndogo linaweza kuwa tatizo kubwa.

HITIMISHO:

Kujifunza zaidi kuhusu kisukari bonyeza hii link hapa chini: https://isayafebu.com/ugonjwa-wa-kisukari/

Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.