- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Jinsi Ya Kuondoa Sumu Mwilini.
Jinsi Ya Kuondoa Sumu Mwilini.
Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.
Leo tujifunze jinsi ya kuondoa sumu mwilini kwa kitaalamu kama Full body cleansing. Ungana nami katika somo hili.
Kwa kusafisha mwili na kuondoa sumu mara kwa mara, mwili wako utaanza kujiponya wenyewe, kuzuia magonjwa, kuwa imara zaidi na himilivu kuliko unavyoweza kudhani~Dr. Edward Group III
Kwa kawaida unapotaka kupaka rangi nyumba hauanzi tu kupaka juu ya rangi mbovu. Unabandua ile rangi iliyochoka ili upate nafasi ya kuanza kupaka rangi mpya. Ndivyo na miili yetu inavyofanya kazi pia.
Unapotaka kuanza kuneemesha mwili, yakupasa kuusafisha kwanza kwa kutoa sumu na taka zote ambazo ni kikwazo cha mwili kufanya kazi vyema.
Hii ni hatua maalum kabisa ya kutoa sumu ndani ya mwili kabla ya kuanza maisha mapya.
Njia rahisi ya kutoa sumu mwilini ni kubadili namna unavyokula na maisha kwa ujumla. Fanya mambo yafuatayo na utaweza kuondoa sumu mwilini kiasilia.
Punguza au acha kabisa pombe
Kula vizuri: Punguza sukari na vyakula vya kubumba
Kunywa maji mengi
Tumikisha mwili utoe jasho
Punguza msongo wa mawazo
Pumzika na lala vya kutosha
Kula vyakula vya kutoa sumu mwilini: Kale, kabeji nyekundu, spinachi, tufaa, tangawizi, zabibu, asali n.k.
MCHANGANYIKO WA KUTOA SUMU MWILINI.
Mahitaji.
Spinach
Dafu
Tango
Tufaa
Tangawizi
Limao
¾ ya kikombe cha maji ya dafu (maji)
Tufaa (apple) za kijani 2
½ ya tango
½ fungu la spinachi au giligilani fungu 1
Tangawizi 1 kubwa
Limao 1 (maji na maganda yake)
Kikombe 1 cha barafu
Maelekezo.
Weka mahitaji yote kwenye blenda yako kwa kuanza na vimiminika kwanza. Anza kusaga taratibu na usage mpaka iwe laini. Ikilainika, unaweza kuchuja kama unahitaji, japokuwa sikushauri kuchuja maana utapoteza nyuzinyuzi na viini lishe vingine vya muhimu. Kunywa hivyo hivyo, utapata madini zaidi.
Tumia mchanganyiko huu kwa wiki 2, asubuhi na jioni
Kwa sababu upo kwenye zoezi la kutoa sumu mwilini, hakikisha unakunywa maji ya kutosha kusafisha mwili. Namaanisha maji ya kutosha kulingana na mahitaji ya mwili.
Baada ya wiki 2 basi unaweza kuendelea na programu nyingine za chakula n.k.
Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu isayafebu.com
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.