- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Je Mwanaume Anaweza Kuugua PID?
Je Mwanaume Anaweza Kuugua PID?
Mwanaume hawezi kupata PID… Lakini mzigo wa PID ya mwenzi wake mara nyingi humuangukia kimya kimya.
Huu si uvumi—ni hali halisi katika mahusiano mengi ya sasa.
Jana usiku nilipokea ujumbe mzito kutoka kwa kijana mmoja aliyekuwa na hofu na mawazo mengi…
Ujumbe wake ulikuwa hivi…
“Daktari, nimekuwa na wasiwasi sana. Mpenzi wangu amekuwa na harufu mbaya ukeni na chupi yake ina ute wa rangi ya njano. Kila tukifanya tendo la ndoa nabaki nikiwa na hofu ya kuambukizwa.Nikipendekeza twende hospitali anachukia sana. Naomba unisaidie kuelewa huu ni ugonjwa gani.”
Hili ni tatizo linalomuumiza mwanamke kiafya na mwanaume kisaikolojia…
PID (Pelvic Inflammatory Disease)
Ni maambukizi yanayopanda kwenye kizazi cha mwanamke na kuathiri mfuko wa uzazi, mirija ya mayai na ovari.
Chanzo mara nyingi ni magonjwa ya zinaa kama Chlamydia au Gonorrhea ambayo huingia kimya bila dalili za haraka.
Dalili ambazo mwanamke anaweza kupitia:
Ute wa njano au kijani
Harufu kali isiyo ya kawaida ukeni
Maumivu ya chini ya tumbo
Maumivu wakati wa tendo la ndoa
Kwa mwanaume:
Hawezi kuugua PID moja kwa moja, lakini anaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa kutoka kwa mwenzi aliyeathirika, na kuanza kupata dalili kama:
Maumivu wakati wa kukojoa
Kuwashwa au kuungua sehemu za siri
Kuvimba korodani
Maambukizi ya njia ya mkojo
PID ni ugonjwa unaovunja mahusiano kisirisiri—mwanamke anaumia mwilini, mwanaume anaumia moyoni.
Ikiachiwa bila matibabu, PID husababisha:
Ugumba
Maumivu ya nyonga yasiyokoma
Hatari ya mimba nje ya kizazi
Kuongezeka kwa mimba kuharibika
Wito kwa wanaume:
Ukiona mabadiliko kwa mwenzi wako, mtoe hofu, sio lawama.
Mshawishi kwa upendo, si kwa hasira.
Mpendekeze kwenda kufanya vipimo mapema.
Wito kwa wanawake:
Usione aibu kutafuta matibabu.
PID hutibika kabisa ikigundulika mapema.
Afya yako ni muhimu kuliko kuhofia lawama.
Elimu, uaminifu, na hatua za haraka ndizo kinga ya kwanza ya mahusiano yenye afya.
Kwa msaada wa matibabu ya asili (kunywa+kunawia ukeni) ya ugonjwa wa pid kwa wanawake wasiliana nasi kwa simu namba 0625305487.