• Dr. ISAYA FEBU Newsletter
  • Posts
  • Hii Nayo Ni Miongoni Mwa Sababu Inayokufanya Mwanaume Unashindwa Kufurahia Tendo La Ndoa kwenye Mahusiano Yako.

Hii Nayo Ni Miongoni Mwa Sababu Inayokufanya Mwanaume Unashindwa Kufurahia Tendo La Ndoa kwenye Mahusiano Yako.

Miongoni mwa sababu inayopelekea baadhi ya wanaume kushindwa kufurahia tendo la ndoa kwenye mahusiano yao ni pamoja na ugonjwa wa pid kwa wenzi wao.

Kwa kawaida mwanaume haumwi PID..Lakini anaumia kimyakimya kwa sababu ya PID ya mpenzi wake. 

Hii siyo hadithi ya mtu mmoja, ni ukweli unaoishi katika ndoa na mahusiano mengi ya sasa…

Jana jioni nilipokea ujumbe mzito kutoka kwa kijana mmoja aliyejaa hofu na sintofahamu...

Na Nukuu Ujumbe Wake…

“Doctor... kuna jambo linaninyima raha kabisa. Mpenzi wangu anatoa harufu mbaya sana ukeni, na kwenye chupi yake kuna uchafu wa njano, Kila tukishiriki tendo la ndoa, najikuta sina amani kabisa, Niko kwenye hofu kubwa ya kuambukizwa, Mbaya zaidi, nikimwambia, ananijia juu kwa hasira, Naomba msaada, ni ugonjwa gani huu?”

Hili si jambo la kupuuzia....

Ni ugonjwa hatari wa mfumo wa uzazi kwa mwanamke, lakini madhara yake huwatesa kimya wanaume pia...!

PID (Pelvic Inflammatory Disease)... 

Ni maambukizi ya bakteria wanaoathiri kizazi cha mwanamke— Mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi (fallopian tubes), na mayai (ovaries)....

Visababishi vikuu ni magonjwa ya zinaa kama Gonorrhea na Chlamydia, yanayoingia bila dalili za haraka....

Matokeo yake...? 

Mwanamke hupata uchafu wa njano au kijani, harufu kali ya uke, maumivu ya tumbo, na wakati mwingine maumivu wakati wa tendo la ndoa...

Mwanaume hawezi kuugua PID, lakini anaweza kuambukizwa madhara ya zinaa kutoka kwa mwanamke aliyeathirika na hata kupata maambukizi ya korodani au mkojo...

 (PID ni miongoni mwa magonjwa yanayobomoa mahusiano kimya kimya) 

Mwanamke anaumia ndani kwa ndani, lakini mwanamume huathirika kisaikolojia, kimwili, na kiakili...

 Na ikiwa haitatibiwa mapema, PID...

Husababisha ugumba, maumivu ya kudumu ya nyonga, na hata mimba kuharibika na mimba za nje ya kizazi. (ectopic pregnancy) ...

NB: Wito kwa wanaume, Kama unahisi mabadiliko haya kwa mwenzi wako, usinyamaze...

Ongea kwa upendo, mshauri mkafanye vipimo hospitalini...

Wito kwa wanawake, Usiogope, usione haya, PID hutibika mapema na kupona kabisa...

Pamoja tukemee magonjwa ya uzazi kwa elimu sahihi na uamuzi wa kwenda hospitali kwa wakati..