- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Faida Ya Kunyonyesha Kwa Akina Mama waliojifungua.
Faida Ya Kunyonyesha Kwa Akina Mama waliojifungua.
Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.
Leo tujifunze kuhusu faida anayoipata mama kwa kunyonyesha baada ya kujifungua. Ungana nami katika somo hili.
Tafiti zinaonyesha unyonyeshaji husaidia kupunguza uwezekano wa aina fulani ya SARATANI hasa;
1) Saratani ya matiti (breast cancer)
2) Saratani ya shingo ya kizazi (cervical cancer)
3) Saratani ya ovari (ovarian cancer)
Hivyo kadri mama anavyomnyonyesha mwanae kwa muda mrefu ndivyo hatari ya kupata Saratani ya matiti hupungua.
Lakini pia kwa ujumla, kunyonyesha ni njia bora ya kutoa lishe, kinga ya afya, na kuimarisha uhusiano wa kimwili na kihisia kati ya mama na mtoto.
usomapo ujumbe huu usisahau pia kushare kwa wale uwapendao ili nao wapate kujifunza.
Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: HOME | ISAYA FEBU
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.