- Dr. ISAYA FEBU Newsletter
- Posts
- Baadhi ya watu wana changamoto ya kusikia kishindo kikubwa kama radi wakati wa kulala au wanapoamka.
Baadhi ya watu wana changamoto ya kusikia kishindo kikubwa kama radi wakati wa kulala au wanapoamka.
Hello habari yako, natumaini unaendelea vizuri.
Je wajua,
Baadhi ya watu wana changamoto ya kusikia kishindo kikubwa kama radi wakati wa kulala au wanapoamka.
Exploding head syndrome
Tatizo hili linajulikana kwa kitaalamu kama “Exploding head syndrome (EHS)”.
Exploding Head Syndrome (EHS) ni hali ambayo mtu anahisi sauti kubwa ya mlipuko au kelele nyingine kali katika kichwa chake bila kuwepo kwa sababu ya nje ya sauti hiyo.
Ni hali isiyo hatari lakini inaweza kuwa ya kusumbua sana.
Hali hiyo ni adimu kutokea na mara nyingi haichagui umri au jinsia na sababu yake haijulikani kabisa, ingawa inaweza kuhusishwa na mabadiliko katika mfumo wa neva au msongo wa mawazo.
Ni muhimu kuzungumza na daktari ikiwa unapata hali hii ili kupata ufafanuzi na msaada.
HITIMISHO
Kujifunza zaidi kuhusu afya tembelea tovuti yangu: HOME | ISAYA FEBU
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu, nikutakie siku njema.